Kiponosakan

Kiponosakan ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Waponosakan kwenye kisiwa cha Sulawesi. Mwaka wa 1981 idadi ya wasemaji wa Kiponosakan imehesabiwa kuwa watu 3000 lakini idadi imepungua sana tangu pale, maana yake lugha ya Kiponosakan imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiponosakan iko katika kundi la Kifilipino.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search